Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema wachezaji wenye asili ya uvivu watapata tabu sana kufanya kazi naye.
Kocha huyo raia wa Uingereza,amesema mara nyingi amekuwa na urafiki wa karibu na watu wachapakazi.
"Kama ni mvivu, utapata matatizo makubwa sana.Kuwa mvivu ni kujiangusha kimaendeleo," alisema Kerr.
Kocha huyo alionyesha mfano kweli yeye si mvivu baada ya siku ya kwanza tu kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe kutimua mbio na wachezaji waliokuwa wakizunguka uwanja.
0 comments:
Post a Comment