728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 02, 2015

    MKWASA ATEMA NYOTA WATANO STARS IKIELEKEA UGANDA

                                    Tokeo la picha la CHARLES MKWASA                          
    KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewaengua wachezaji watano katika kikosi chake kinachoondoka leo jioni kwenda Kampala kum
    enyana na wenyeji, Uganda mwishoni mwa wiki.

    Stars itakuwa mgeni wa Korongo wa Uganda Jumamosi Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2016 Rwanda.

    Na Mkwasa amewaengua beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kiungo Abdi Banda wote wa Simba SC kwa sababu ni majeruhi, wakati Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu na Andrew Vincent wa Mtibwa Sugar wameachwa kwa sababu za kiufundi na Mwadini Ally wa Azam FC ni mgonjwa.

     Mkwasa ameteua wachezaji 20 wanaoondoka jioni ya leo kwenda Kampala, ambao ni makipa; Mudathir Khamis (KMKM) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga), mabeki ni Juma Abdul (Yanga), Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC) na Hassan Isihaka (Simba SC).

    Viungo ni Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Simba SC) na Deus Kaseke (Mbeya City).
    Washambuliaji ni John Bocco (Azam FC), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ali (Mtibwa Sugar).

    Mara baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kurithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuatia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kwanza na Uganda, Mkwasa alitaja kikosi wachezaji 26 na kuwa nacho kambini kwa wiki moja hoteli ya Kiromo, Bagamoyo huku mazoezi akifanya uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.

    Mbali na wachezaji hao, benchi la Ufundi litaongozwa na Mkwasa, Mshauri wake wa Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, Msaidizi wake Hemed Morocco, kocha wa makipa, Manyika Peter, Mtunza Vifaa Hussein Swedi ‘Gaga’, Meneja Omar Kapilima pamoja na Mratibu Msafiri Mgoyi. Stars inatakiwa kushinda 4-0 Jumamosi ili kusonga mbele CHAN.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKWASA ATEMA NYOTA WATANO STARS IKIELEKEA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top