Gueye:Aston Villa imefikia makubaliano na klabu ya Lille kuhusu kumnunua kiungo Msenegal Idrissa Gueye,25 kwa ada ya £9m Idrissa Gueye (Sky sources)
Remy:Chelsea imeachana
na mpango wa kumuuza mshambuliaji wake Mfaransa Loic Remy ambaye anawindwa vikali na vilabu vya Swansea, West Ham na Crystal Palace (Daily Mirror)
Van Persie:Mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi Pierre van Hooijdonk amesema klabu ya Manchester United inajaribu kumuuza kwa siri mshambuliaji wake Robin Van Persie baada ya mwezi januari kutaka kumpeleka Fenerbahce (Daily Mirror)
Gaitan:Atletico Madrid itaziba nafasi ya Arda Turan kwa kumsajili winga wa Benfica Nico Gaitan,mwenye thamani ya €35m.(Marca)
Llorente:Kocha wa Real Madrid Rafa Benitez amewaambia mabosi wa klabu hiyo wamsajili mshambuliaji wa Juventus Muhispania Fernando Llorente,30.(La Sexta)
Coates:Sunderland imefanikiwa kumsajili moja kwa moja mlinzi wa Liverpool aliyekuwa klabuni hapo kwa mkopo Sebastian Coates,24.Coates amesaini mkataba wa miaka mitatu baada ya klabu ya Sunderland kuridhishwa na kiwango chake.
Turan:Vilabu vya Barcelona na Atletico Madrid vimefikia makubaliano juu ya usajili wa winga na kiungo Arda Turan, 28.Barcelona itamsajili Turan kwa ada ya chini ya €41m.(Sport)
Diaby:Kiungo aliyetemwa na Arsenal Abou Diaby,29 amewasili Texas Marekani kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu ya FC Dallas inayoshiriki ligi ya MLS.
De Gea:Manchester United imeripotiwa kupunguza bei ya mlinda mlango wake David De Gea inayewindwa na Real Madrid toka €46m mpaka €35m.(Inside Football)
0 comments:
Post a Comment