728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 18, 2016

    EURO 2016:UBELGIJI YATOKA USINGIZINI NA KUICHAPA IRELAND TATU SAAAAFI

    Bordeaux,Ufaransa.

    MABAO mawili ya Romelu Lukaku na moja la Axel Witsel yameipa Ubelgiji ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ireland Kaskani katika mchezo wa Kundi E uliochezwa katika uwanja Matmut Atlantique stadium,Bordeaux jioni ya leo.

    Romelu Lukaku alianza kuifungia Ubelgiji bao la kwanza dakika ya 47 kwa mkwaju mkali baada kupokea pasi kutoka kwa Kevin De Bruyne.Ubelgiji iliandika bao la pili kupitia kwa kiungo wake Axel Witsel aliyefunga kwa kichwa dakika ya 61akiunganisha krosi ya mlinzi Thomas Meunier.

    Lukaku aliifungia Ubelgiji bao la tatu dakika ya 70 ya mchezo baada ya kupokea pasi toka kwa nahodha Eden Hazard. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO 2016:UBELGIJI YATOKA USINGIZINI NA KUICHAPA IRELAND TATU SAAAAFI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top