Dar es Salaam,Tanzania.
Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi leo alikutana na secretariat ya Yanga chini
ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake madarakani Bw. Clement Sanga na
Katibu Mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit kwa ajili ya kujadili mustakabali wa uchaguzi wa Yanga ambao uliingia katika mvutano na TFF pamoja na BMT.
Maamuzi yaliyotoka ni kwamba,uchaguzi wa Yanga umebarikiwa kuendelea kama ulivyopangwa na kamati
ya uchaguzi ya Yanga kwamba utafanyika June 11, 2016 chini ya uangalizi wa kamati ya uchaguzi ya TFF.
Wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo ambao walichukua fomu TFF, kikao kimeamua kiwarudishe kamati ya uchaguzi ya Yanga kuendelea na taratibu zilizopo za uchaguzi endapo wanakidhi vigezo vya uchaguzi vya kamati ya uchaguzi ya Yanga.
0 comments:
Post a Comment