728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 07, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI JUMANNE YA LEO JUNI 7,2016

    Roy Hodgson 

    Hodgson:Kocha wa England Roy Hodgson amewaambia wachezaji wake kusahau kuhusu vilabu vyao,usajili na badala yake waweke mawazo yao katika michuano ya Euro inayotarajiwa kuanza Ijumaa ya wiki hii.Pia Hodgson ameripotiwa kuwapiga marufuku wachezaji wake kufanya mawasiliano yoyote yale na mawakala wao mpaka hapo michuano ya Euro itakapokuwa imekwisha. (Daily Mirror )

    Nonga:Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wameripotiwa kuwa tayari kumpiga bei mshambuliaji wake Mtanzania Paul Nonga kwenda klabu yoyote ile ikiwa dau la Tsh 40m litawekwa mezani kama fidia ya gharama ilizotumia kumsajili nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Mbeya City na Mwadui FC.(Binzubery)

    Herrera:Kwa mujibu wa mwahabari wa Mexico, Vladimir Garcia Liverpool wamekaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Porto Mmexico Hector Herrera,26, lakini huenda ikapambana na upinzani toka kwa AS Napoli ambayo imeripotiwa kujiandaa kutuma ofa ya €18m (£14.1million) na mshahara wa £150,000 kwa wiki.(Sports)

    Zinchenko:Manchester City imeshinda mbio za kumuwania mshambuliaji kinda wa Ufa,Oleksandr Zinchenko.Zinchenko,19, atasaini mkataba wa kuichezea Manchester City baada ya kuitumikia Ukraine katika michuano ya Euro.(Sports)

    Mendy:Leicester City imetuma ofa ya €10 kwenda Nice kwa ajili ya kutaka kumsajili kiungo wake wa ulinzi Nampalys Mendy, 23 ili kuchukua nafasi ya NG'olo Kante anayetaka kuhama klabuni hapo.Taarifa za ndani zinasema tayari Leceister City imeshakubaliana kila kitu na Mendy,22,lakini Nice inataka day zaidi.(RMC Sport)

    King:Kiungo wa Leicester City Andy King amesema nguvu/ari iliyopo klabuni hapo haiwezi kudorora hata kama Jamie Vardy ataamua kujiunga na Arsenal.Tuko wachezaji 25 kikosini lakini kama mmoja/wawili wanaamua kuondoka tunawatakia kheri,mapambano yanaendelea.(Daily Mail)

    Chambers:Mlinzi kinda wa Arsenal Calum Chambers,21, ameripotiwa kukaribia kujiunga na Watford kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja hii ni baada ya kushinda kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mfaransa Arsene Wenger.(Daily Mail)

    Vardy:Arsenal imepata hofu kuwa Jamie Vardy atabadili mawazo na kuamua kubakia Leicester City.Hofu hiyo imekuja baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Fleetwood Town kupaa kwenda Ufaransa bila ya kuiambia chochote klabu hiyo ya Emirates.(Daily Mirror)

    Matic:Manchester United imefanya mawasiliano na Chelsea ili kuangalia uwezekana wa kumsajili kiungo wake Mserbia Nemanja Matic,27.(gianlucadimarzio.com)

    Pjanic:Rais wa AS Roma James Palotta amesema klabu yake haina ubavu wa kumzuia kiungo wake Mbosnia Miralem Pjanic kuhamia Chelsea.(Metro)

    Batshuayi:Barcelona imeripotiwa kuwa itafufua mpango wake wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Marseille Mbelgiji Michy Batshuayi,22,ikiwa itamkosa mshambuliaji wa Celts Vigo Manuel Nolito.(talkSPORT)

    Mkhitaryan:Borussia Dortmund imekiri kushindwa kumshawishi kiungo wake Muarmenia Henrikh Mkhitaryan,27, kusaini mkataba mpya na badala yake itamruhusu kuondoka katika dirisha hili la usajili barani Ulaya.(Mirror)

    Sahin:Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili kwa mara nyingine kiungo wa Borussia Dortmund Mturuki Nuri Sahin.(AMK)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI JUMANNE YA LEO JUNI 7,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top