Barcelona, Hispania.
Klabu ya FC Barcelona kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Michezo,Robert Fernandez imetangaza kuwa mlinzi wake wa kulia Mbrazil Dani Alves da Silva ataihama klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
Fernandez amethibitisha kuondoka kwa Alves,33, mchana wa leo wakati akiongea wa waandishi wa habari na kusisitiza kuwa FC Barcelona inaheshimu uamuzi huo.
Alves alijiunga na FC Barcelona mwaka 2008 akitokea FC Sevilla kwa ada ya €30m akifanikiwa kutwaa mataji sita ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati huohuo habari zinasema Alves huenda akajiunga na Juventus ama Manchester City.
0 comments:
Post a Comment