Victoria, Usherisheri.
Timu ya taifa ya Algeria imekata tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON ya mwaka 2027 huko Gabon baada ya jioni ya leo kuichapa Usherisheri kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa Kundi J uliochezwa katika uwanja wa Stade Linite huko Victoria-Usherisheri.
Mabao yaliyoipa ushindi huo Algeria yamefungwa dakika za 41 na 60 na washambuliaji wake Yassine Benzia na El Arbi Hilal Soudani.
Kwa matokeo hayo Algeria imefanikiwa kufuzu baada ya kufikisha pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara tano,nafasi ya pili inakaliwa na Ethiopia yenye pointi 5 ikiwa imecheza michezo minne.
Algeria itacheza mchezo wake wa mwisho mwezi Septemba kwa kuvaana na Lesotho,Usherisheri wao watasafiri mpaka Addis Ababa kwenda kucheza na Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment