London, England.
England imemaliza maandalizi yake ya kujiandaa na michuano ya Euro 2016 kwa kuichapa Ureno kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Alhamis usiku katika uwanja wa Wembley, London.
Bao lililoipa ushindi huo wa kihistoria England limefungwa kwa kichwa dakika ya 86 na mlinzi Chris Smalling akiunganisha krosi ya winga Raheem Sterling aliyekuwa ameingia akitokea benchi.
Hilo limekuwa ni bao la kwanza kwa Smalling kuifungia England tangu alipoanza kuichezea miaka kadhaa iliyopita.Mpaka sasa Smalling ameichezea England michezo 25.
Katika mchezo huo Ureno ambayo ilikuwa bila ya nahodha wake Cristian Ronaldo ilipata pigo dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinzi wake Bruno Alves kulimwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi mshambuliaji wa England Harry Kane.
England itasafiri mpaka Ufaransa tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Euro 2016 dhidi ya Urusi Juni 11 huko Marseille.
0 comments:
Post a Comment