Manchester, England.
Klabu ya Manchester City imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Mjerumani Ilkay Gundogan toka Borussia Dortmund kwa ada ya £21m.
Gundogan,25,amesaini mkataba wa miaka minne na ataanza kuwatumikia matajiri hao wa jijini la Manchester Julai Mosi mwaka huu.
Kiungo huyo wa zamani wa Nuremberg amekuwa ni mchezaji wa kwanza kujiunga na Manchester City tangu klabu hiyo imteue Muhispania Pep Guardiola kuwa kocha wake mpya akichukua nafasi ya Mchile Manuel Pellegrini aliyemaliza mkataba.
Gundogan anaiacha Borussia Dortmund akiwa ameifungia mabao 15 katika jumla ya michezo 157 ya Bundesliga na mashindano mengine.
0 comments:
Post a Comment