728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 02, 2016

    MACHINJIO YA BRITANNIA YABADILISHWA JINA

    Stoke,England.

    ULIOKUWA Uwanja wa nyumbani wa Klabu ya Stoke City,Britannia, Jana Jumatano Juni 1,ulibadilishwa jina na sasa unafahamika kama bet365 Stadium.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya Stoke City kupata udhamini mnono wa miaka sita toka katika kampuni ya michezo ya kubashiri ya bet365.Com ambayo pia ni mmiliki wa klabu hiyo kongwe zaidi England.

    Mbali ya kupewa jina hilo jipya uwanja huo pia utapanuliwa na kuongezwa viti 1,800 na kufanya uwe na uwezo wa kuchukua zaidi ya watazamaji 30,000 walioketi.Kwa sasa uwanja wa bet365 Stadium unachukua watazamaji zaidi ya 29,257.

    Uwanja wa Britannia ama Machinjioni kama wengi walivyopenda kuuita ulijipatia umaarufu mkubwa kwa wapenzi wa Ligi Kuu ya England kutokana na kuwa mmoja kati ya viwanja vigumu sana kwa vilabu vigeni kupata matokeo mazuri hasa yale ya pointi tatu huku wachezaji wakiumizwa vibaya na timu mwenyeji.

    Stoke City ilianza kuutumia uwanja wa Britannia mwaka 1997 baada ya kuhama uwanja wa Victoria Ground.

    Pichani:Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey akipewa huduma ya kwanza baada ya kuvunjwa mguu,Britannia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MACHINJIO YA BRITANNIA YABADILISHWA JINA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top