Manchester, England.
KOCHA Jose Mourinho yupo tayari kuuza hadi wachezaji 13 wa kikosi cha kwanza Manchester United kwa mujibu wa El Confidencial .
Meneja mpya wa United ameripotiwa kukutana na Mkurugenzi Ed Woodward Ijumaa kujadili mipango yake ya usajili kuelekea kampeni za 2016/17 na
ameorodhesha msururu wa wachezaji ambao hawana tija.
Juan Mata, Ander Herrera na Memphis Depay wanaongoza katika orodha,
wakati Bastian Schweinsteiger, Marouane Fellaini, Ashley Young, Michael Carrick,Marcos Rojo na Sergio Romero wapo katika hatari ya kuuzwa.
Hata mustakabali wa Luke katika Old Trafford yupo hatarini kutemwa, ipo wazi
kwamba Mourinho anataka kumtoa kwa mkopo baada ya kukosa karibu msimu
mzima kwa kuvunjika mguu. MustakabaliI a Antonio Valencia na Matteo Darmian upo shakani hali kadhalika.
Mchezaji mmoja tu ndo hayupo kwenye hatari ya kuoneshwa mlango wa kutokea,David De Gea ambaye inafahamika kuwa Mourinho anataka kumbakisha Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment