Dortmund, Ujerumani.
Baada ya kupokwa wachezaji wake kwa kipindi kirefu Borussia Dortmund hatimaye leo imejibu mapigo baada ya kufanikiwa kumsajili kiungo Mjerumani Sebastian Rode toka Bayern Munich kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
Rode,25,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuichezea miamba hiyo ya Signal Iduna Park baada ya kufuzu vipimo vya afya jioni ya leo.
Kabla ya kutua Bayern Munich,Rode aliichezea Eintracht Frankfurt.Mpaka anaiacha Bayern Munich Rode amefanikiwa kuanza michezo 11 katika kipindi cha misimu miwili aliyokaa Allianz Arena.
Rode anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Borussia Dortmund.Wengine ni Marc Bartra,Ousmane Dembele na Mikel Merino.
0 comments:
Post a Comment