Dar es Salaam,Tanzania.
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC leo Jumatatu wamemsajili aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa Tanzania Prisons ya Mbeya Beno Kakolanya,22, na kumpa kandarasi ya miaka miwili.
Kakolanya ambaye pia ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha timu
ya Taifa Taifa Stars,amesaini kuichezea Yanga SC akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake katika klabu ya Tanzania Prisons inayomilikiwa na Jeshi la Magereza Tanzania.
Kakolanya ambaye alianzia soka lake katika Akademi Mbaspo ya Mkoani Mbeya anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Yanga SC tangu pazia la ligi kuu Bara lilipofungwa.Wengine ni Hassani Kessy toka Simba SC na Juma Mahadhi toka Coastal Union ya Tanga.
0 comments:
Post a Comment