Kurt Zouma.
Vardy:Mshambuliaji Muingereza Jamie Vardy,29,ameomba apewe muda zaidi wa kuamua iwapo ahamie Arsenal ama abaki Leceister City.(Metro)
Deeney:Leicester City wametuma ofa ya £15m kwenda Watford kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Muingereza Troy Deeney ili kuja kuwa pacha wa Jamie Vardy ambaye wanaamini atachomoa kuhamia Arsenal.Msimu uliopita Deeney,27,alifunga mabao 13 Ligi Kuu England.(The Daily Telegraph)
Walcott:West Ham United imeripotiwa kuwa tayari kutoa £25m ili kumsajili winga wa Arsenal Theo
Walcott.Habari zinasema Wakala anayeshughulikia dili la Walcott ndiye huyo huyo anayeshughulikia dili la Jamie Vardy kuhamia Arsenal.( Standard Sport)
Zouma:Beki wa Chelsea Mfaransa Kurt Zouma amesema hafikirii kuungana na Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United licha ya kocha huyo kuhusishwa na mpango wa kutaka kusajili nyota kadhaa wa Chelsea wakiwemo Nemanja Matic na Willian.(MYTF1)
Konoplyanka:Leicester City imeanza kuulizia uwezekano wa kumsajili winga wa Sevilla Yevhen Konoplyanka ili kujiandaa na michuano ya Klabu bingwa Ulaya.(Estadio Deportivo)
Asamoah: Juventus imeripotiwa kuwa tayari kumruhusu kiungo wake Mghana Kwadwo
Asamoah,27, kujiunga na Chelsea.(Gazzetta dello Sport)
Slimani: Sporting Lisbon imeripotiwa kuwa itaikataa ofa ya €20m toka Leicester City kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake Mualgeria Islam Slimani,27,lakini iko tayari kumwachia endapo dau la €30m litawekwa mezani.( A Bola)
Koeman:Everton imekubali kuipa Southampton £5m kama fidia ya kutaka kumnyakuwa kocha wake Mholanzi Ronald Koeman,53.(Daily Mail)
0 comments:
Post a Comment