728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 19, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 19,2016

    Daley Blind

    Blind:Arsenal imepania kufanya makubwa msimu ujao na katika kuona hilo linafanikiwa imeanza jitihada za kutaka kumsajili staa wa Manchester United mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani,Mholanzi Daley
    Blind.Arsenal imeamua kumgeukia Blind,26, baada ya kuona kuwa staa huyo wa zamani wa Ajax atakuwa na wakati mgumu wa kupata namba Old Trafford hasa baada ya ujio wa mlinzi Eric Bailly kutoka Villarreal.(Mirror)

    Mane:Southampton haitaki kuona winga wake mahiri Msenegal Sadio Mane,23, anaondoka klabuni hapo na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa imepandisha bei yake mpaka kufikia £40m kama mbinu ya kuvivunja nguvu vilabu vyote vinavyomtaka staa huyo wa zamani wa Redbull Salzburg.(The Sun)

    Bonucci:Meneja wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho ameonyesha kuvutiwa na mlinzi wa Juventus, Leonardo Bonucci,29, na ameripotiwa kutaka kumsajili kwa dau la £25m.(Daily Star)

    Wenger:Arsenal iko tayari kumpa mkataba mpya wa miaka miwili meneja wake Mfaransa Arsene Wenger,66.(Mirror)

    Dzeko:Sunderland imechoka kuwa timu ya kukoswa koswa kushuka daraja karibu kila msimu na tayari imetuma ofa ya €11m kwenda AS Roma kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester City,Mbosnia Edin Dzeko lakini italazimika kutoa kitita cha €15m ili kuishawishi miamba hiyo ya Estadio Olympic.(gianlucadimarzio.com)

    Kovacic:Liverpool imeungana na vilabu vya Juventus, Roma na AC Milan kuwania kumsajili kwa mkopo kiungo wa Real Madrid,Mcroatia Mateo Kovacic,22.(Sky Sport Italia)

    Nolito:Mwenyekiti wa Celta Vigo, Carlos Mourino amesema staa wa klabu hiyo Muhispania Manuel Arago maarufu kama Nilito,29, anaweza kuihama klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili kwa ada ya €18m (£13.8m).




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 19,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top