Paris,Ufaransa.
TIMU za taifa za Romania na Uswisi zimeshindwa kutambiana baada ya leo jioni kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo mkali wa Kundi A wa michuano ya Euro 2016 uliochezwa katika uwanja wa Parc des Princes jijini Paris.
Romania ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za Uswisi dakika ya 18 ya mchezo baada ya Bogdan Stancu kufunga kwa mkwaju wa penati .
Mkwaju huo ulitolewa baada ya nahodha wa Uswisi Stephan Lichtsteiner kumvuta jezi ndani ya box Alexandru Chipciu.
Bao la Uswisi limefungwa dakika ya 57 na Admir Mehimedi na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya bao 1-1.
0 comments:
Post a Comment