Marseille, Ufaransa.
TIMU ya taifa ya Ufaransa "Les Blues" imekuwa timu ya kwanza kufuzu katua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 baada ya usiku wa leo kuichapa Albania kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo mkali wa Kundi A uliochezwa Stade Velodrome, Marseille.
Mabao yaliyoipa Ufaransa ushindi huo muhimu yamefungwa dakika za 90 na 95.Bao la kwanza la Ufaransa limefungwa kwa kichwa na mshambuliaji Antoine Griezmann akiunganisha krosi safi ya mlinzi Adil Rami toka wingi ya kulia na bao la pili limefungwa na kiungo Dimitri Payet kwa mkwaju mkali wa karibu baada ya kuuwahi mpira uliomponyoka mshambuliaji Andre Pierre Gignac.
Kwa matokeo hayo Ufaransa imefanikiwa kuongoza Kundi A baada ya kufikisha pointi katika michezo miwili,Uswisi ni ya pili ikiwa na pointi zake nne.Nafasi ya tatu imeshikwa na Romania yenye pointi moja na mkiani wako Albania ambao hawana pointi yoyote licha ya kushuka dimbani mara mbili.
0 comments:
Post a Comment