728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 18, 2016

    EURO 2016:HISPANIA YAIDUNDA UTURUKI NA KUTINGA 16 BORA

    Nice,Ufaransa.

    HISPANIA imeendelea kuonyesha kuwa bado inautaka Uchampioni wa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo hii ni baada ya usiku huu kuichapa Uturuki kwa mabao 3-0 Katika mchezo wa kundi D uliochezwa katika dimba la Allianz Riviera/Stade de Nice ,mjini Nice.

    Hispania ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza baada ya Alvaro Morata kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Manuel Agudo "Nolito". 

    Bao la pili limefungwa dakika ya 37 na Manuel Agudo "Nolito" huku bao la tatu na la mwisho likifungwa na Alvaro Morata dakika ya 48 na kuifanya Hispania itoke uwanjani kifua mbele kwa mabao hayo 3-0.

    Kwa ushindi huo Hispania imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kufikisha pointi sita katika michezo miwili.Nafasi ya pili inashikiliwa na Croatia yenye pointi nne,Czech iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja huku Uturuki ikiwa mkiani baada ya kushinda kupata pointi yoyote.

    VIKOSI

    Hispania: David De Gea, Juanfran Torres,Sergio Ramos, Gerard Pique, Jordi Alba,Sergio Busquets, Andres Iniesta, Cesc Fabregas, David Silva, Manuel "Nolito" Agudo,Alvaro Morata

    Uturuki: Volkan Babacan, Gokhan Gonul,Mehmet Topal, Hakan Balta, Caner Erkin,Ozan Tufan, Selcuk Inan, Oguzhan Ozyakup,Hakan Calhanoglu, Burak Yilmaz, Arda Turan



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO 2016:HISPANIA YAIDUNDA UTURUKI NA KUTINGA 16 BORA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top