Dundo,Angola.
YANGA SC imefuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika licha ya jioni kufungwa bao 1-0 na Sagrada Esperansa katika mchezo mkali wa marudiano wa hatua ya mtoano.
Bao pekee la mchezo huo uliotawaliwa na fujo toka kwa wenyeji Sagrada Esperanca limefungwa dakika ya 24 na Love Kabungula.
Katika mchezo huo Yanga SC ilimaliza pungufu baada ya nahodha wake Nadir Haroub kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Shukrani za dhati zinapaswa zimuendee mlinda mlango Deogratius Munish aliyedaka penati ya Love Kabunguka atika dakika za lala salama na kuipeleka Yanga SC mpaka hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Katika mchezo mwingine mabingwa wa michuano hiyo Etoile du Sahel ya Tunisia imefuzu licha ya kufungwa bao 1-0 na Mounana ya Gabon.Katika mchezo wa Kwanza Sahel ilishinda kwa mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment