728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 20, 2016

    SAMATTA AIONGOZA GENK KUUA 5-2 UBELGIJI

    GENK,UBELGIJI

    Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta Alhamis Usiku ameiongoza Klabu yake ya KRC Genk kuibuka na Ushindi mnene wa mabao 5-2 dhidi ya Klabu ya Anderletch katika mchezo mkali wa Raundi ya tisa ya hatua ya mtoano ya kuwania kufuzu michuano ya Europa Ligi kwa timu za Ubelgiji.

    Katika mchezo huo uliopigwa huko Genk katika dimba la Cristal Arena na Samatta kucheza kwa dakika zote 90,Wageni Anderletch ndiyo walikuwa wa Kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Filip Djuricic kufunga dakika ya 25.Dakika ya 45 Leon Bailey alifanikiwa kuifungia KRC Genk bao la kusawazisha na kufanya miamba hiyo iende mapumziko ikiwa sare ya bao 1-1.

    Kipindi cha pili Marcos Suarez aliipa Anderletch kuongozi baada ya kuifungia bao la pili dakika ya 60 hata hivyo bao hilo halikudumu kwani dakika ya 65' T. Buffel aliwazidi ujanja walinzi wa Anderletch na kuisawazishia KRC Genk.

    KRC Genk ilifanikiwa kuongeza mabao mengine dakika za 76,78 na 90 kupitia kwa' A. Pozuelo,W. Ndidi na N. Karelis na kufanya mchezo uishe kwa wenyeji KRC Genk kupata ushindi wa mabao 5-2 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya Europa Ligi msimu ujao.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAMATTA AIONGOZA GENK KUUA 5-2 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top