728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 16, 2016

    MCHEZO WA MAN UNITED NA BOURNEMOUTH KUCHEZWA KESHO JUMANNE,MASHABIKI KUINGIA BUREEEEE KABISA.

    MANCHESTER, ENGLAND.

    MCHEZO wa Ligi Kuu England uliopangwa kuchezwa Jana Jumapili kati ya wenyeji Manchester United dhidi ya wageni Bournemouth na kuahirishwa kutokana na hofu ya kuwepo kwa bomu katika Uwanja wa Old Trafford sasa utachezwa kesho Jumanne Mei 17 katika uwanja huohuo mishale ya Saa 4:00 Usiku.

    Wakati huohuo Uongozi wa Manchester United umetangaza kuwa mashabiki wa timu zote mbili waliokuwa tayari na tiketi za mchezo huo watarudishiwa fedha zao na sasa wataingia bure kabisa bila ya kutozwa chochote.

    Manchestet United itaingia katika mchezo wa kesho ikiwa na nafasi finyu ya kufuzu michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao kwani itahitaji kuifunga Bournemouth kwa jumla ya mabao 19-0 ili iweze kuwaondoa katika nafasi ya nne wapinzani wao wa jadi Manchester City ambao ambao wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

    Jumapili jioni Manchester City ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Swansea City huko Liberty,Wales.Manchester City ilitangulia kupata bao kupitia kwa Kelechi Iheanacho na wenyeji Swansea City kusawazisha kupitia kwa Andre Ayew.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MCHEZO WA MAN UNITED NA BOURNEMOUTH KUCHEZWA KESHO JUMANNE,MASHABIKI KUINGIA BUREEEEE KABISA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top