728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 16, 2016

    MASHABIKI WACHOMA MOTO UWANJA BAADA YA TIMU YAO KUSHUKA DARAJA

    Eskisehirspor,Uturuki.

    Mashabiki wa klabu ya Eskisehirspor wameuchoma moto uwanja wao wa nyumbani wa Eskisehir Atatürk Stadium baada ya klabu yao kushuka mpaka daraja la pili kufuatia kuchapwa mabao 2-1 na klabu ya Medipol Basaksehir katika mchezo wa Ligi daraja la kwanza nchini Uturuki.

    Mashabiki hao waliokasirishwa na matokeo hayo waliuvamia uwanja huo uliojengwa mwaka 1953 punde tu baada ya mwamuzi kumaliza mchezo na kuanza kuuchoma moto huku wakibomoa vitu mbalimbali vilivyokuwa uwanja hapo.

    Sehemu zilizoathirika zaidi ni sehemu ya kuchezea (pitch),majukwaa,viti,ofisi na mabango ya biashara.Wakati huohuo taarifa kutoka nchini Uturuki zinasema katika ghasia hizo mashabiki watatu wa Eskisehirspor walijeruhiwa vibaya na kulazimika kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.

    Licha ya mashabiki hao kufanya uharibifu huo lakini inaweza isiwe pigo sana kwani tayari Eskisehirspor ilikuwa ikitarajiwa kuuhama uwanja huo baada ya mchezo huo na kuhamia katika uwanja mpya wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 33,000.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MASHABIKI WACHOMA MOTO UWANJA BAADA YA TIMU YAO KUSHUKA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top