728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 16, 2016

    YANGA SC YAENDA ANGOLA BILA YA NYOTA WAKE WANNE

    Dar es salaam,Tanzania.

    YANGA SC imeondoka leo alfajiri kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa mchujo wa kuwania kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika bila ya nyota wake wanne.

    Nyota walioachwa katika safari hiyo ya Angola ni pamoja na Benedicto Tinocco, Said Juma Makapu,Issoufou Boubacar na Malimi Busungu aliye majeruhi.

    Yanga SC itashuka dimbani siku ya Jumatano huko Luanda,Angola kuvaana na wenyeji wao Sagrada Esperanca.Katika mchezo huo Yanga SC inahitaji ushindi ama sare yoyote ile ili iweze kutinga hatua ya makundi.

    Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja Wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita Yanga SC ilipata ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa kipindi cha pili na Simon Msuva na Matheo Antony.

    KIKOSI KILICHOONDOKA LEO NI;

    Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.

    Mabeki; Juma Abdul, Mwinyi Haji,Oscar Joshua, Vincent Bossou,Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Nahodha Nadir Haroub' Cannavaro'.

    Viungo; Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.

    Washambuliaji; Donald Ngoma,Matheo Anthony, Amissi Tambwe na Paul Nonga.

    BENCHI LA UFUNDI;

    Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm,Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi,Kocha wa makipa; Juma Pondamali
    Daktari; Edward Bavu,Mchua Misuli; Jacob Onyango,Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo na Meneja; Hafidh Saleh

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAENDA ANGOLA BILA YA NYOTA WAKE WANNE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top