728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 01, 2016

    MAN UNITED YAIAMBIA LECEISTER CITY KATANGAZIE UBINGWA WAKO KWINGINE SIYO OLD TRAFFORD,YAIBANA NA KUTOKA NAYO SARE YA 1-1

    Manchester, England.

    Manchester United imegoma kuona Leceister City ikitangazia ubingwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford baada ya kuibana na kutoka nayo sare ya kufungana bao 1-1 jioni ya leo mbele ya watazamaji 75,275.

    Manchester United ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 8 tu ya mchezo baada ya Antony Martial kufunga kwa mkwaju wa chini chini akiunganisha krosi ya mlinzi Antonio Valenciai

    Dakika ya 17 mpira wa adhabu uliopigwa kiungo Danny Drinkwater ulitua kichwani kwa nahodha Wes Morgan na kuifungia Leceister City bao la kusawazisha.

    Dakika ya 86 Leceister City ilipata pigo baada ya kiungo wake Danny Drinkwater kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumwangusha Memphis Depay.

    Kwa matokeo hayo Leceister City itabidi isubiri matokeo ya mchezo wa kesho Jumatatu kati ya Chelsea na Tottenham au michezo miwili ya mwisho ndipo itangaze ubingwa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN UNITED YAIAMBIA LECEISTER CITY KATANGAZIE UBINGWA WAKO KWINGINE SIYO OLD TRAFFORD,YAIBANA NA KUTOKA NAYO SARE YA 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top