London,England.
Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson leo mchana ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 26 kitakachoiwakilisha nchi hiyo katika michuano ijayo ya Ulaya [Euro 2016] itayoanza kutimua vumbi lake Juni 10 huko nchini Ufaransa.
Katika kikosi hicho kitakachopunguzwa na kubaki na wachezaji 23 kinda wa Manchester United Marcos Rashford,18 amejumuishwa kwa mara ya kwanza baada ya kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu England.Akifanikiwa kufunga mabao saba katika michezo 16.
Mbali ya Rashford nyota wengine waliojumuishwa ni Andros Townsend wa Newcastle,Jack Wilshere wa Arsenal naye amejumuishwa licha ya kucheza michezo mitatu pekee ya Ligi Kuu msimu huu.Theo Walcott,Phil Jagielka na Leighton Baines wameachwa.
Kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kinatarajiwa kutangazwa Mei 30 baada ya England kumaliza michezo yake ya kirafiki dhidi ya Uturuki na Australia.
KIKOSI KAMILI
0 comments:
Post a Comment