Dar es salaam,Tanzania.
AMEVURUGWA? Unaweza kujiuliza swali hili baada ya habari za uhakika
kutoka ndani ya Klabu ya Azam FC kudai kwamba kocha wao mkuu hataiongoza
timu yao kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yanga utakaopigwa Juni
11 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msimu ujao benchi la ufundi la Azam linatarajia kuongozwa na makocha
wapya ambao watachukua nafasi zitakazoachwa na Stewart na msaidizi wake
Denis Kitambi ambao uongozi wa klabu hiyo umepanga kuachana nao.
Tayari makocha hao wapya, Zeben Hernand ambaye atakuwa kocha mkuu na
msaidizi wake Jonas Luis wamekwishatua nchini wakisubiri kuanza kazi ya
kuinoa timu hiyo.
Stewart alitangaza kuachia ngazi kukinoa kikosi cha timu hiyo baada
ya ligi kumalizika, ambapo kikosi chake kitacheza mechi ya mwisho Mei 21
kitakapoivaa Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mwingereza huyo ameiwezesha Azam kutinga hatua ya fainali ya FA,
lakini hataiongoza kwenye mchezo dhidi ya Yanga baada ya mabosi wake
kuwaleta nchini Waispania hao.
Chanzo cha habari kilisema Stewart huenda akakosekana kwenye benchi
la ufundi la timu hiyo itakapocheza na Yanga na badala yake litaongozwa
na Luis.
“Stewart atawaaga wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Mgambo, kocha
mpya ataanza kazi kwenye mchezo wa fainali ya FA, kwani tayari amekiona
kikosi cha timu hiyo baada ya kukishuhudia kilipocheza na African
Sports,” alisema.
0 comments:
Post a Comment