Dar es Salaam,Tanzania.
Kampuni ya Airtel Tanzania jana Ijumaa Mei 20, 2016 imekutana na
Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa
mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya
umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ambaye ndio aliongoza kikao
hicho, alitoa shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la
vijana ambalo ndio msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. “Naamini ya
kwamba kwa kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika
mbali kwa kupata matokeo mazuri.”
Tangu kuanzisha kwa michuano ya Airtel Rising Stars miaka mitano
iliyopita, soka la vijana nchini imekuwa na mafanikio makubwa“Leo, Timu
ya Taifa chini ya miaka 20 – Serengeti Boys, imeundwa na vijana ambao
wamekuwa ni chimbuko la Airtel Rising Stars,” alisema Selestine na
kuongeza kuwa hata timu ya Taifa ya Wanawake – Twiga Stars, Klabu za
Liguu na zile zinazoshiriki ligi daraja ya kwanza, zinatumia wachezaji
ambao wamekuzwa kwa michuano ya Airtel Rising Stars.
Airtel imeweza kuiwezesha TFF kufika maeneo ambayo yamekuwa ni vigumu
kufika kutafuta vipaji. Kwa kufanya hivyo, tuweza kupata vijana wenye
vipaji vingi na hata kwa sasa hivi, baadhi yao wako na Timu ya Taifa ya
Vijana Serengeti kushiriki michuano ya Kimataifa inayoendelea India,
alisema Mwesigwa.
Katibu Mkuu huyo wa TFF aliomba Airtel kuendelea kudhamini miradi ya
soka ya vijana kwa vile ndio njia pekee Tanzania inaweza kuwa na timu
bora na imara ya Taifa. Nchi nyingi zinazofanya vizuri kwenye michuano
mbali mbali ya soka ni kwa vile waliweza kuwekeza kwenye program mbali
mbali za vijana kama vile Airtel Rising Stars. Kwa kushirikiana na
nyinyi, tutaweza kupata na kukuza vipaja vya soka ambazo watakuwa na
msaada mkubwa kwenye timu ya Taifa.
Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano Airtel Tanzania, Jackson Mmbando
alisema “kampuni yake itaendelea kudhamini program za soka la vijana
ambazo zimeweza kuwa na mafanikio makubwa kwa miaka mitano iliyopita.
Lengo letu ni kuwa na timu ya taifa bora kama vile Misri, Cameron,
Nigeria, Ivory Coast na Ghana,” alisema Mmbando huku akisisitiza njia
pekee ya kufikia mafanikio hayo ni kuwekeza na kukuza soka la vijana.
Airtel pia imetoa shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Habari,
Michezo na Sanaa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa
ushirikiano wao ambao umeifanya Airtel Rising Stars kuwa moja ya
mashindano yenye mafanikio makubwa hapa Tanzania. Bila ushirikiano na
serikali pamoja na wadau wa soka hapa nchini, Airtel Rising Stars
hangeweza kufika hapa ilipo kwa leo, alisema Mmbando.
Mmbando alisema kwa mwaka huu, Tanzania haitashiriki kwenye michuano
ya kimataifa ambayo huleta pamoja wachezaji waliong’ara kwenye nchi zao
Barani Afrika kwa ajili ya kubadilisha uzoefu, bali itashirikiana na TFF
kuweka mikakati mingi zaidi ya kuwawezesha vijana hawa kufanya vyema
hata baada ya mashindano ya Airtel Rising Stars kwisha.
0 comments:
Post a Comment