Na Thomas Sauli
Fid q msanii wa hip hop bongo aliwahi kuimba mstari mmoja katika moja ya nyimbo zake kua "maua hunyauka story huisha, kumbukumbu husahaulika hii dunia inamaanisha sisi sote tunapita"
Hapa Fid q kwa upeo wangu alimaanisha kwamba maisha ni mapito na kwamba dunia haisimami hivyo mabadiliko ni jambo muhimu
Maisha yanakwenda kasi sana juz juz tuu ilikua 2000 lakini sasa ni 2015 lakini kocha Arsene Wenger haendi sawa na kasi ya maisha katika soka bado yupo katika fikra za mwaka 2000 bado anaamini timu ya Sanogo, Flamin, Akpom, Monreal na Meterceker inaweza kumletea mataji
Wenger anasumbuliwa na dhambi ya kukariri kwamba mafanikio alopata zamani atayapata kwa mfumo ule ule, bado lengo lake kuu ni no 4 badala ya ubingwa.
Wenger ni miongon mwa makocha ambao hana muda wa kuangalia mifumo ya wapinzani wake ndio maana tangu nimfahamu sijawahi kumuona kahudhuria mechi za wapinzani wake badala yake yeye anaendesha timu kwa mifumo ile ile ambayo ni rahisi kusomwa na wapinzani
Dunia inahitaji mabadiliko wakati wote ndio maana kila binadamu ana mwisho wake na sasa imefika mwisho wa kocha Arsenal Arsene Wenger kuendelea kufundisha Arsenal.
Arsenal kwa kifupi inahitaji kocha mwenye changamoto mpya ambaye atakwenda sawa na kasi ya timu pinzani ambazo zinasajili wachezaji bora kila kukicha
Mi nafikir Wenger bado yupo pale Arsenal kwa sababu ya historia lakini kuhusu makombe kwa sasa nadhani hata umpe Messi na Ronaldo bado Arsenal itakua mbovu
Wenger kwa sasa sidhan kama ni sahihi kuwepo cha kufanya kwake ni kuondoka na kupisha mtu mwingine hii itamjengea heshima la sivyo kumbu kumbu na story zake zitasahaulika na ataondoka kwa aibu.
0 comments:
Post a Comment