London,England
Mlinzi na nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry jana aliweka pembeni kwa muda machungu ya kubugizwa goli 5-3 na klabu ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa ligi kuu na kumwagia sifa nyota wa mchezo huo mshambuliaji wa Spurs Harry Kane.
Terry amesema
``Kane ni mchezaji mgumu na msumbufu sana kukabiliana nae.Ni mchezaji aina ya Sergio Aguero,Alexis Sanchez na Robbin Van Persie.
Ni mchezaji msumbufu kuwahi kukutana nae,nimekutana na wachezaji wengi lakini Kane kiboko.
Kama ataendelea kujituma namna hii na kujifunza zaidi sina shaka kuwa atakuwa ni kati ya nyota wakubwa hapo baadae"Alimaliza Terry.
Kane aliifungia Spurs magoli mawili na kusababisha penati iliyofungwa na winga Andre Townsend katika mchezo ulioshudia Chelsea ikiuanza mwaka kwa kipigo cha mbwa mwizi.
0 comments:
Post a Comment