728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 02, 2015

    KWAHERI MTUMISHI STEVEN GERRARD

    Liverpool,England.

    Sasa ni rasmi kuwa mtumishi mwema Steven Gerrard (34) hatoitumikia tena jezi nyekundu ya klabu ya Liverpool kama ilivyozoeleka pindi msimu huu utakapo fikia tamati yake hapo mwezi Mei.

    Baada ya sintofahamu na maswali ya hapa na pale juu ya hatma ya kiungo Steven  Gerrad kama ataendelea kuwepo Liverpool ama ataondoka ili kuzipisha damu changa zichukue nafasi Anfield,taarifa kutoka kwake na makao makuu ya klabu leo ijumaa zinasema sasa ni rasmi Gerrad ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu.

    Mtumishi anaondoka. Hatutoyaona tena yale mashuti yake makali makali yaligeuka shubiri kwa makipa wa timu pinzani.Mtumishi huyu mwenye moyo wa ajabu,moyo wa kijasiri,moyo usiochoka kupambana hatoibusu tena ile nembo ya the cop,hatouimba tena ule wimbo wa ``U will never walk alone" akiwa mchezaji wa Liverpool na kitambaa chake mkononi (Arm band) pindi mei itakapokuwa imefika.Mtumishi anakwenda kule ambako hata yeye mwenyewe amekiri hajui ni wapi.

    Akitangaza uamuzi huo Gerrard amesema...

    ``Huu umekuwa ni uamuzi mgumu sana kuuchukua,mimi na familia yangu tumejadili hili kwa kipindi kirefu sasa.

    Nataka kucheza nje mbali kabisa.Mbali ambako haitotekea nikaingia uwanjani kuvaana na Liverpool.Siwezi kuhimili kucheza dhidi ya Liverpool.

    Maamuzi yangu yanatokana na hamu ya kutaka kupata changamoto mpya za kimaisha sehemu nyingine na ninataka kuhakikisha kuwa ninakuwa sina cha kujutia pindi soka yangu itakapokuwa imefika mwisho.

    "Kutoka sasa mpaka mwisho wa msimu,nitaendelea kuitumikia Liverpool kwa moyo wangu wote kama ambavyo nimekuwa nikiitumikia."

    Gerrard,alizaliwa huko Merseyside,Liverpool katika kijiji kiitwacho
    Whiston.Alijiunga na shule ya soka ya Liverpool akiwa na umri wa miaka minane na kufanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza akitokea benchi dhidi ya klabu ya  Blackburn
    Rovers hii ikiwa ni  Novemba1998.

    Gerrard ameifungia Liverpool
    jumla ya magoli180 katika michezo 695 yakiwemo mawili aliyofunga siku ya mwaka mpya dhidi ya Leceister City.Mwaka 2005 Gerrard  aliiongoza Liverpool  kutwaa ubingwa wa Ulaya dhidi ya klabu ngumu ya Ac Milan baada ya kufunga goli la kwanza katika mchezo ambao Liverpool walitoka nyuma na kupata sare ya goli 3-3 na mwisho Liverpool kushinda kwa mikwaju ya penati.

    Gerrard ametwaa taji moja la Uefa Cup,mataji mawili ya FA Cup,mataji matatu ya Carling Cup,Ngao ya jamii na mataji mawili ya Uefa Super Cup pia amefanikiwa kuichezea timu ya taifa ya England jumla ya michezo  114 kabla ya kutundika daruga baada ya fainali za kombe la dunia zilizopigwa huko Brazil mwaka 2014 maarufu kama Brazuka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KWAHERI MTUMISHI STEVEN GERRARD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top