Milan,Italia.
Ikiwa ni siku mbili tu tangu kufunguliwa kwa
dirisha la usajili barani ulaya timu ya soka ya
Inter milan imeonekana kuanza mwaka vyema
kwa kuweka sawa safu ya ushambuliaji kwa
kumsajili mshambuluaji wa Arsenal Lukas
Podolski.
Mjerumani huyo mshindi wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 29
anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Inter Milan iliyo chini ya Kocha Roberto Mancini.
Podolski alitua Milan jana ijumaa na leo jumamosi atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuivaa Juventus siku ya jumanne katika mchezo wa ligi ya Seria A.
Podolski anatumia Inter kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita ambao utaiingizia Arsenal kitita cha €600,000 kama ada ya uhamisho ambayo inaweza kupanda na kufikia €850,000 ikiwa Inter itafuzu michuano ya Europa na ikiwa Inter itafuzu ligi ya mabingwa
Arsenal itavuna €1milioni.
Baada ya kutua Inter Podolski amesema
``Nimeongea na kocha Manchini.Nadhani ni kocha mzuri.
Simfahamu vizuri lakini naifahamu vyema ligi ya Seria A.Nataka kuisaidia timu ifuzu ligi ya mabingwa"
0 comments:
Post a Comment