London,England.
Baada ya wiki iliyopita kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho kutoa shutuma kwa mwamuzi Mark Taylor kuwa aliinyima penati timu yake na kumlima kadi ya manjano kiungo wake Cesc Fabregas matokeo yaliyopelekea vijana wake kutoka sare ya goli 1-1 na klabu ya Southampton na kudai kuwa kuna kampeni chafu ya kuhakikisha Chelsea haichukua ubingwa wa Epl.
Safari hii kocha huyo amekuja na mpya na hii ikiwa ni muda mfupi tu tangu aiongoze klabu yake kupokea kipigo kizito cha goli 5-3 toka kwa Tottenham Hot Spurs amekudai kuwa kiungo wake Eden Hazard halindwi vya kutosha na marefa kitendo ambacho kitafanya nyota huyo afikirie kuhama England.
Mourinho amemueleza refa aliyechezesha mcheza huo Phil Dowd kuwa ni mtu aliye taratibu mno na kudai alishindwa kuendana na kasi ya mchezo kitendo kilichopelekea ashindwe kuona madhambi aliyofanyiwa Hazard na mlinzi wa Spurs Federico Fazio.
Mourinho amesema ``Watu wa nchi hii wanaopenda mpira,wanapaswa kumpenda pia Eden Hazard,”
Ameongeza “Kwa namna,mchezo baada ya mchezo,anavyoadhibiwa na wapinzani na asivyolindwa na waamuzi,huenda iko siku Eden Hazard akalazimika kuondoka na kwenda kucheza soka kwingine.
0 comments:
Post a Comment