Vyombo vikubwa vya habari vya England asubuhi ya leo karibu vyote vinaripoti habari ya kuhama kwa nyota wa Arsenal Lukas Podolski 29.
Baadhi ya vyombo hivyo ni magazeti ya Daily Mail,Mirror na Daily Telegraph ambayo yamepambwa na habari kubwa isemayo Podolski kuhamia Inter Milan ndani ya saa 48 zijazo.
Habari ya Podolski kuondoka imepata uzito mkubwa baada ya kuenea uvumi kuwa nyota huyo alishambuliana kwa maneno makali na kocha Arsene Wenger na kisha akajiondoa katika kikosi kilicho safari na kwenda kuambulia kichapo cha goli 2-0 toka kwa Southampton jana jioni.
Inasemekana Inter Milan itamsajili Podolski kwa mkopo wa miezi sita kisha kumnunua moja kwa moja hapo mwisho wa msimu kwa kitata cha €6.5m.
Podolski anaondoka Arsenal baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza akiwa ni chaguo la tatu nyuma ya Oliver Giroud na Danny Welbeck.
0 comments:
Post a Comment