Kocha wa Arsenal Arsene Wenger leo amekiona cha moto baada ya shabiki mmoja wa klabu hiyo kumvamia wakati mchezo wa ligi kuu dhidi ya Southampton ukiendelea.
Shabiki huyo ambaye jina lake halijafahamika alishuka toka jukwaani na kusogea mahali alipokaa kocha Wenger na kuanza kumtolea maneno makali huku akionyesha ishara ya kumtaka kocha huyo aondoke.Hata hiyo mtu huyo aliondolewa na askari kabla hali haijawa balaa zaidi katika mchezo ambao Arsenal ililala kwa goli 2-0.
Hili ni tukio kubwa na la aina yake kumtokea kocha huyo ambaye wiki kadhaa nyumba alivamiwa na kutukanwa na mashabiki wa klabu hiyo wakati akijiandaa kupanda treni kurudi London baada ya kikosi chake kubugizwa magoli 3-2 na klabu ya Stoke City.
0 comments:
Post a Comment