Na Thomas Sauli,
Mwaka mwingine unakatika ni saa mbili asubuhi tumebakiwa na masaa tuimalize 2014 dunia ina mengi ndani yake.
Miaka inakata Arsenal ikiwa chini ya kocha Arsene Wenger kip kikubwa ambacho kinasababisha wenger awepo ? Mi nadhani mafanikio alopata zaman ndio yanamuweka pale pamoja na mapato anayoingizia timu.
Bado mashabiki wa Arsenal duniani kote wanapokea mwaka 2015 lakini moyoni bado wana wasi wasi na timu yao hii ni kwa sababu ya kiwango kibovu kinachooneshwa na Arsenal chini ya wenger.
Bado Wenger anatumia mbinu za kizamani katika soka la kisasa hajabadilika bado ni mgumu wa kubadili mifumo hata timu ikicheza chini ya kiwango ameshindwa kuzifunga timu kubwa pale Epl na bado anaota ubingwa
Kitu kingine amekua hafanyi usajil sahihi kwa wakati sahihi. Amekua hawatumii baadhi ya wachezaj wazuri ndani ya kikos mfano Podolsk na Campbell badala yake anamtumia mchezaji ambaye hata Bunley hapati nafas na si mwingine ni Sanogo
Kwa timu ilivyo na aina ya wachezaji alionao pamoja na mifumo anayotumia Wenger hawez kuipa Arsenal mafanikio hata apewwe miaka 10
Arsenal ni timu kubwa sana duniani lakini Wenger anaiiendesha kama timu ndogo hapa ndo tunamaanisha Wenger kwa Arsenal ni kama injini ya Vitz inayojaribu kuendesha scannia hebu tusubir tuone.
0 comments:
Post a Comment