Kiungo David Silva ametanabaisha kuwa kucheza na timu zilizoko mkiani mwa ligi ni vigumu kuliko kucheza na timu zilizoko juu.
Silva ameyasema hayo baada ya hivi karibuni klabu yake ya Manchester City kujikuta ikitoka sare ya mogoli 2-2 dhidi ya klabu iliyoko mkiani ya Burnley tena nyumbani Etihad stadium.
Silva ambaye timu yake leo ina kibarua kigumu itakapo kutana na klabu nyingine ya Sunderland iliyoko chini anasema..
``Ni balaa kweli kama Burnley walivyothibitisha,
kila mchezo ni mgumu kwenye Premier League na msimu ni mrefu mno.”
“Timu yoyote ile inaweza kukufunga kama hauko katika kiwango kizuri.Naamini kucheza na timu zilizo chini ni balaa kuliko kucheza na timu zilizoko juu kwa sababu zinacheza kila mchezo kama ndiyo mchezo wake mwisho wa msimu.
“Tunahitaji kujipanga tena ili kurudi na hatimaye kuanza kushinda tena baada ya kuendelea kujutia pointi tulizozipoteza dhidi ya Burnley”
0 comments:
Post a Comment