728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 07, 2017

    Samatta afunga,aasisti Genk ikishinda 2-1 nyumbani


    Genk,Ubelgiji.

    MBWANA Samatta (Kulia) akishangilia kwa staili ya kusujudu baada ya usiku huu kuifungia Genk bao moja na na kuasisti jingine katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Eupen kwenye mchezo mkali wa kusaka tiketi ya kuwania kucheza michuano ya Europa Ligi msimu ujao.

    Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Luminus Arena huko Genk,Jere Uronen aliifungia Genk bao la kuongoza katika ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa 
    Mbwana Samatta.


    Dakika kumi baadae,katika dakika ya 28 Mbwana Samatta aliifungia Genk bao la pili akitumia vyema pasi ya nahodha Tomas Buffel aliyetangazwa nyota wa mchezo huo.Bao la wageni Eupen limefungwa na Mnigeria Henry Onyekuru katika dakika ya 76.

    Aidha katika mchezo huo Genk ililazimika kucheza ikiwa pungufu baada ya Jere Uronen kutolewa nje katika dakika ya 78 kwa mchezo mbaya.

    Ushindi huo umeifanya Genk iendee kujitanua kileleni mwa kundi A baada ya kufikisha pointi 19 kufuatia kushuka dimbani mara 7.Eupen iko nafasi ya tano ikiwa na pointi 7.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Samatta afunga,aasisti Genk ikishinda 2-1 nyumbani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top