728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 07, 2017

    Timu ya Thomas Ulimwengu yaendeleza unyonge ligi kuu Sweden


    Soedra,Sweden.

    TIMU ya AFC Eskilstuna inayochezewa na Mtanzania,Thomas Ulimwengu imeendelea kuonyesha unyonge kwenye ligi kuu ya soka nchini Sweden baada ya jioni ya leo ikiwa ugenini huko Stadsparksvallen kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Joenkoepings Soedra .

    AFC Eskilstuna ambayo imepanda daraja la ligi kuu msimu huu ilijikuta ikiwa nyuma katika dakika ya 47 ya kipindi cha pili baada ya Darly Smylie kuifungia Joenkoepings Soedra bao pekee na la ushindi .Dzenis Kozica alishindwa kuifungia Joenkoepings Soedra bao la pili baada ya kukosa mkwaju wa penati katika dakika ya 62.

    Kichapo hicho kimeiacha AFC Eskilstuna mkiani mwa msimamo mwa ligi kuu Sweden yenye timu 16 baada ya kuambulia pointi tatu pekee katika michezo saba iliyocheza mpaka sasa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Timu ya Thomas Ulimwengu yaendeleza unyonge ligi kuu Sweden Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top