728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 07, 2017

    Wenger apata ushindi wa kwanza dhidi ya Mourinho,Arsenal ikiichapa Man United 2-0 Emirates


    London, England.

    HATIMAYE Arsene Wenger amepata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Jose Mourinho baada ya jioni hii kuongoza vyema Arsenal kuifunga Manchester United mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu ya England ulioisha hivi punde kwenye dimba la Emirates jijini London.

    Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Andre Marriner ilishuhudiwa timu zikienda mapumziko zikiwa zimeshindwa kufungana.

    Mabao yaliofuta uteja wa muda mrefu wa Wenger kwa Mourinho yamefungwa dakika ya 54 na kiungo Granit Xhaka aliyefunga kwa mkwaju mkali wa mbali uliomgonga kiungo Ander Herrera na kumpoteza maboya mlinda mlango David De Gea kabla ya kutinga wavuni.

    Tokeo la picha la arsenal 2-0 man united

    Bao la pili limefungwa na Danny Welbeck kwa kichwa katika dakika ya 57 akiunganisha vyema krosi safi kutoka kwa Alex Oxlade Chamberlain aliyemzidi ujanja beki wa kulia wa Manchester United Matteo Darmin na kumimina majalo safi kwa mfungaji.

    Tokeo la picha la arsenal 2-0 man united

    Ushindi huo umeifanya Arsenal isalie katika nafasi ya sita ikiwa imejikusanyia pointi 63 katika michezo 34.Manchester United imebaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 65 katika michezo 35.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wenger apata ushindi wa kwanza dhidi ya Mourinho,Arsenal ikiichapa Man United 2-0 Emirates Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top