728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Yanga SC yamruka mzungu wa Azam FC


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Yanga SC kupitia kwa katibu wake mkuu,Charles Boniface Mkwasa wamekana kuwa katika mazungumzo na kocha wa zamani wa Azam FC,Mwingereza Stewart John Hall kwa ajili ya kuja kuchukua mikoba ya Mzambia,George Lwandamina "Chicken.

    Akifanya mazungumzo na waandishi wa habari mtaa wa Twiga na Jangwani yalipo makao makuu ya klabu hiyo,Mkwasa amesema habari hizo ni uzushi wa mitandaoni na watu wasio na nia njema na klabu hiyo.

    Mkwasa amesisitiza Yanga hawana mpango wowote na kocha huyo wala kocha yoyote kwa sasa na kuongeza kuwa hizo ni chokochoko na wanazipinga vikali.

    " Timu yetu kwa sasa inaongoza ligi na tupo katika njia nzuri ya kuutetea ubingwa wetu. Hawa wanaoleta maneno ya uzushi hawana nia njema na klabu , wanataka watu waache kufanya kazi ili malengo yao yatimie .

    Klabu haipo katika mpango ambao moja kwa moja ni hasara kwa klabu kuanza kulipa fidia na kupoteza malengo yake ." Kwa sasa Hall ni kocha mkuu wa Gor Mahia ya Kenya.

    Mkwasa pia amewaomba Watanzania na wapenzi wa soka kiujumla kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumamosi kuipa sapoti timu hiyo pale itakaposhuka Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuvaana na MC Alger kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

    "Tunahitaji kushinda hapa nyumbani ili kupunguza ugumu wa mechi ya ugenini , hivyo sapoti yenu itakuwa ni msingi mzuri wa morali kwa vijana"



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga SC yamruka mzungu wa Azam FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top