728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Ghana yapata kocha mkuu mpya


    Accra,Ghana.

    GHANA imemteua kwa mara nyingine mzawa,James Kwesi Appiah kuwa kocha mkuu mpya wa timu yake ya taifa,Black Stars.

    Kwesi,56,aliyekuwa akicheza nafasi ya ulinzi wa kati katika enzi zake za usakataji kabumbu amepewa mkataba wa miaka miwili na ataanza kibarua hicho Mei 1 mwaka huu.

    Kwesi amepata kibarua hicho baada ya kuibuka kidedea mbele ya beki wa zamani wa Ufaransa,Willy Sangol pamoja na mzawa Maxwell Kanodu aliyekuwa kocha wa muda wa Ghana tangu Machi mwaka huu baada ya Muisrael, Avram Grant kumaliza mkataba wake.

    Mbali ya Kwesi,wengine waliopata vibarua vipya ni mlinda mlango wa zamani wa Ghana,Richard Kingston yeye ameteuliwa kuwa kocha wa makipa huku nahodha wake wa zamani Stephen Appiah akiteuliwa kuwa meneja wa timu.

    Jukumu la kwanza alilopewa Kwesi ni kuhakikisha Ghana inafuzu michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 huko Urusi pamoja na michuano ya AFCON ya mwaka 2019.

    Hii ni mara ya pili Kwesi anakabidhiwa mikoba ya kuinoa Black Stars mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo alihudumu kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya mwaka 2014 kujiuzulu baada ya Ghana kufanya vibaya kwenye fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil ambapo ilimaliza mechi zake za makundi ikiwa mkiani.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ghana yapata kocha mkuu mpya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top