728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Simba SC dimbani leo Uwanja wa shule ya Msingi Waja


    Geita.

    LEO Jumatano mabingwa wa zamani wa ligi kuu bara,Simba SC watashuka kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Waja ulioko wilayani Geita mkoani Mwanza kucheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji wao Geita Gold Sports.

    Simba SC ambao tangu juzi Jumatatu jioni walianza kambi yao wilayani hapo wakitokea mkoani Kagera walipochapwa mabao 2-1 na Kagera Sugar wanataka kuutumia mchezo dhidi ya Geita Gold Sports kwa ajili ya kujiwinda na michezo yao miwili iliyobaki ya kanda ya ziwa dhidi ya Mbao FC Aprili 10 na Toto African Aprili 15.

    Kuelekeo mchezo huo wachezaji wa Geita Gold Sports kwa nyakati tofauti wametamba kuifunga Simba SC na kuwapa raha mashabiki wao waliokosa michezo mikubwa kwa kipindi kirefu kutokana na timu hiyo kunyimwa kupanda ligi kuu bara baada ya kukumbwa na kashfa ya upangaji wa matokeo.

    Kwa sasa Simba SC wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu bara wakiwa na alama 55 alama moja nyuma ya wapinzani wao Yanga SC wenye alama 56 katika nafasi ya kwanza.







    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba SC dimbani leo Uwanja wa shule ya Msingi Waja Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top