728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 09, 2017

    Tunisia yamtimua kazi Kasperczak


    Tunis,Tunisia.

    TUNISIA imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu yake ya taifa Mpolandi,Henry Wajelech Kasperczak.

    Kasperczak mwenye umri wa miaka 70 alipewa jukumu la kuinoa Tunisia Julai 2015 akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbelgiji,Georges Leekens.

    Kufutwa kazi kwa Kasperczak kumekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Tunisia imepoteze michezo yake miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Cameroon na Morocco.

    Kasperczak atakumbukwa baada ya mwezi Januari kuifikisha Tunisia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya AFCON kabla ya kutolewa na Burkina Faso.

    Chama cha soka cha Tunisia (TFF) kimesema kocha mpya atatangazwa mwishoni mwa mwezi huu.

    Jukumu la kocha huyo mpya litakuwa ni kuhakikisha Tunisia inafuzu fainali za kombe la mwakani kitakalofanyika nchini Urusi pamoja na zile za AFCON za mwaka 2019 mbele ya mataifa kama Misri, Niger na Swaziland.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Tunisia yamtimua kazi Kasperczak Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top