Miami,Marekani.
MSWISI Roger Federer sasa
atamvaa mpinzani wake wa siku nyingi Rafael Nadal wa Hispania kwenye mchezo wa
fainali wa michuano ya wazi ya tenesi ya Miami baada ya alfajiri ya kuamkia leo kupata
ushindi wa kishindo wa seti mbili kwa moja dhidi ya Nick Kyrgios wa Australia
katika mchezo mkali wa nusu fainali.
Katika mchezo huo uliochezwa kwa masaa matatu ilishuhudiwa Federer,35, akiibuka kidedea kwa ushindi wa seti 7-6, 6-7 na 7-6 dhidi ya Kyrgios,21.Katika nusu fainali nyingine Nadal,30, alimshinda Fabio Fognini,29, kwa seti mbili bila za 6-1 na 7-5.
Nadal hajawahi kushinda ubingwa wa michuano hiyo licha ya kuwahi kufika fainali mara nne mwaka 2005,2008,2011 na 2014.Federer yeye ameshinda ubingwa huo mara mbili mwaka 2005 na 2006.Mwaka 2005 akimfunga Nadal kwenye fainali.Wawili hao watakutana kwenye finali kesho Jumapili huku huo ukiwa ni mpambano wao wa 38.Mwaka huu wamekutana mara moja kwenye michuano ya wazi ya Australia na Ferderer kuibuka mbabe.
0 comments:
Post a Comment