Faridi Miraji,Dar es salaam.
Mshambuliaji wa timu ya KRC Genk inayoshiliki ligi kuu nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta ametajwa kwenye mipango ya timu kubwa tatu za nchini Ujerumani.
Vilabu hivyo ni Wolfburg, Humburger na Borrusia Monchenglabach vyote vinataka kumsajili Samatta anayekadiriwa kuwa na thamani ya Euro million 10.
Samatta mwenye mkataba na KRC Genk hadi 2020 ameripotiwa kuwa ataruhusiwa kuondoka Luminus Arena iwapo tu vilabu hivyo vya Ujerumani vitakubali kutoa kiasi hicho cha fedha.
Samatta alijiunga na KRC Genk Januari 2016 akitokea TP Mazembe ya DR Congo ilimsajili kutoka Simba SC ya Dar Es Salaam,Tanzania.
0 comments:
Post a Comment