Faridi Miraji, Dar es salaam.
Obrey Chirwa amegoma kusafiri na timu kwenda Algeria kuwakabili MC Alger , Hadi kufikia jana Chirwa na Ngoma pekee ambao walikuwa hawajakabidhi passport kwa ajili ya maandalizi ya safari hiyo! Baada ya maelewano Ngoma alikubali kupeleka Passport lakini hali ilikuwa tofauti kwa Chirwa ambaye aliendelea kushikilia msimamo wake, bila kupewa mshahara hatosafiri na timu.
Kitendo hicho kimemkasirisha mno Mzambia mwenzake George Lwandamina kwani hivi karibuni Chirwa amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza.
Katibu mkuu Charles Mkwasa amewatoa hofu Wana Yanga na watanzania wazalendo juu ya kukosekana kwa Chirwa, kwani kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi ambapo kimekuwa kinapata matokeo licha ya baadhi ya (wachezaji muhimu) key players kukosekana.
0 comments:
Post a Comment