728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Yanga SC kuondoka kesho kwenda kuwavaa MC Alger


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                           


    Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake hapo kesho kuelekea Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger

    Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

    Wachezaji watakaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Beno Kakolanya . Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani. 

    Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma

    Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine Zulu,Malimi Busungu,Matheo Antony,Ally Mustapha,Pato Ngonyani ,Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga SC kuondoka kesho kwenda kuwavaa MC Alger Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top