728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Simba SC:Kuna waziri amekuwa akiwapigia simu wachezaji wetu akitaka wajiunge na timu yake


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    TIMU ya Simba SC kupitia kwa Mwenyekiti wa kamatati yake ya usajili,Zacharia Hans Poppe imesema imepata taarifa kuwa kuna waziri mmoja wa Serikali ya awamu ya tano amekuwa akiwavuruga wachezaji wake kwa kuwapigia simu akitaka wajiunge na timu yake.

    Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini hapa leo asubuhi ,mwenyekiti huyo amesema hana sababu ya kutaja jina la waziri huyo kwani anajijua na kuongeza kuwa kitendo hicho ni kibaya sana hasa katika kipindi hiki ambacho timu yao inapambana kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara.

    Pia Hans Poppe amemtaka waziri huyo aliyedai kuwa kwa sasa ana timu mbili moja mpya na moja ya zamani asubiri wachezaji hao wamalize mikataba yao kwanza kisha awapeleke huko anakotaka.

    Amesema "Tayari tuna taarifa juu ya waziri huyo kuwapigia simu wachezaji wetu akitaka wajiunge na timu yake.Tunaomba aache kwani kufanya hivyo kutawavuruga wachezaji wetu na kuwafanya washindwe kutimiza vyema majukumu yao uwanjani.

    Kama anataka kuwasajili wachezaji wetu basi asubiri ligi iishe kisha afuate taratibu stahiki za uhamisho wa wachezaji.Sisi Simba SC hatuna kawaida ya kuzuia wachezaji wetu pindi wanapotaka kuhama ama kutakiwa na timu nyingine.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba SC:Kuna waziri amekuwa akiwapigia simu wachezaji wetu akitaka wajiunge na timu yake Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top