728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Mmachinga:Yanga wana kibarua kigumu Algeria



    James Eduma,Iringa.

    Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Young Africans, Mohamed Hussein Mmachinga amesema bado kikosi cha klabu hiyo kina kazi ya kufanya mbele ya MC Alger katika mchezo wa mkondo wa pili wa  kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika CAF.

    Mmachinga amesema Young Africans walipaswa kutumia nafasi walizozipata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliounguruma mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam, ili kujitengenezea mazingira mazuri ya mchezo ujao, lakini haikuwa hivyo.

    Amesema kuna haja kwa wahusika wa benchi la ufundi la young Africans kubuni mbinu zaidi ambazo zitafanikisha mpango wa kupambana ugenini ambapo anaamini patakua pagumu zaidi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mmachinga:Yanga wana kibarua kigumu Algeria Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top